MAISHA YA SIKU HIZI

[1]
Maisha ya siku hizi dunia giza,
Waume na wanawake iepukeni,
Vijana na wanawali angalieni,
Mungu anayachukia yote ya giza.

[chorus]
Angalia matendo ni ya machukizo,
Epuka wana wa Mungu maovu hayo,
Bali kwa matendo yao wanamkana.
“Angalia” madhehebu yote “hayo” yatoka wapi?
“Yesu Kristo” alijenga kanisa moja duniani.

[2]
Neno la Mungu lasema tusiongeze,
Wala kupunguza unabii wa kweli,
Ole wetu ole wangu tukiongeza,
Atakuja, kila mmoja na ujira wake.

[3]
Jiulize ndugu yangu, wafanya nini?
Kumuasi Mungu kwa matendo maovu?
Wakati ni huu ndugu tubuni dhambi,
Njia, kweli, na uzima ni kwa Mwokozi.