MAGENDO

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

MAGENDO

[1]
Magendo na kuruka, ni mchezo wa laana,
Wana wa Ibilisi na Baba yao Shetani;
Umetokea kuzimu, utazikwa Jehanamu,
Nao umebuniwa, mwisho wa Ulimwengu.

Magendo ya wakubwa watoto na vijana;
Wazee wanaume pia na wanawake;
Magendo inalevya kuliko na vidonge,
Waendao Mbinguni hawashiriki kamwe.
Dada - Jisalimishe Yesu anaponya;
Kaka - Jisalimishe Yesu anaponya;
Baba - Jisalimishe Yesu anaponya;
Mama - Jisalimishe Yesu anaponya.

[2]
Magendo ikichezwa nchi hutetemeka,
Amani inakwisha watu huhangaika,
Maandiko yatimia aliyonena Bwana,
Watapenda pesa sana kuliko roho zao.