KWELI NI HUZUNI

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

KWELI NI HUZUNI

[1]
Kweli ni huzuni kwa kifo chake Bwana Yesu.
Alivyowambwa pale mtini, akasema moyoni
Namaliza kazi kwa huzuni. x2

Akalia - Kwa huzuni
Hata mwisho - Alikufa
Pale juu msalabani
Akakata roho kwa huzuni. x2

[2]
Yesu alisema, “na ninyi mtateswa hivi
Nami nitakuwa ndani yenu hata mle kifoni
Nitawafufua kwa furaha.” x2

[3]
Kweli ni ajabu kwa kifo chake Bwana Yesu
Alivyowambwa pale mtini, akasema na Baba
Baba wasamehe kwa huzuni. x2