Kupigana Vita

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Kupigana Vita

[1]
Kupigana vita nikotayari
Bibilia silaha ya vita
Vita vyake Bwana nitapigana
Kwa nguvu zake mwokozi

[chorus]
(Nipe) Nipe uwezo wako Bwana
(Niwe) Niwe mshindi wa vitani
(Nipa) Nipate kumshinda yule
Mwovu shetani

[2]
Nguvu za shetani tutazishinda
Kama tukimwomba Bwana
Atatupa nguvu tukimshinda
Tukae naye mwokozi

[chorus]
(Nipe) Nipe uwezo wako Bwana
(Niwe) Niwe mshindi wa vitani
(Nipa) Nipate kumshinda yule
Mwovu shetani

[3]
Kuna raha kule kwa Bwana Yesu
Yesu ndiye kiongozi
Tujikaze ndugu kupiga vita,
Njia yetu ni msalaba

[chorus]
(Nipe) Nipe uwezo wako Bwana
(Niwe) Niwe mshindi wa vitani
(Nipa) Nipate kumshinda yule
Mwovu shetani