KUNA MJI WA AMANI

[1]
Kuna mji wa amani, amani ya kweli,
Unapatikana huko, mji wa Sayuni.

Sayuni -Mji wa Baba Sayuni -Mji wa Baba
Sayuni ni masikani ya Baba, nakuomba kwa roho,
Baba unirehemu, nami nikaingie Sayuni.

[2]
Ni Sayuni ya mbinguni, tunakwenda huko,
Ndiko liko pumziko, mji wa Sayuni.

[3]
Bwana Yesu ndiye njia, ya kwenda Mbinguni,
Tukim-fuata yeye tutafika Sayuni.