Kazi Yake Bwana Yesu

[1]
Kazi yake Yesu ilipomalizika
Aliwaita wanafunzi wake
Akawaambia mambo haya yote
Kule Gethsemane

[Chorus]
Yule Yuda kamwambia
Wayahudi akisema
Nitakaye mbusu ndiye huyo
Mkamateni Mkamateni x2

[2]
Neno lake Yesu likawa hivi
Hivi sasa Baba yamemalizika
Ulivyonituma hapa duniani
Nimeyatimiza

[Chorus]
Yule Yuda kamwambia
Wayahudi akisema
Nitakaye mbusu ndiye huyo
Mkamateni Mkamateni x2

[3]
Walikwenda kule kwake Gethsemane
Wakamwona yule Bwana Yesu (Yuda)
Akambusu akamkumbatia
Wakamfungafunga

[Chorus]
Yule Yuda kamwambia
Wayahudi akisema
Nitakaye mbusu ndiye huyo
Mkamateni Mkamateni x2

[4]
Walimpeleka kortini mwa Kayafa
Alihukumiwa kwenda kwa Pilato
Alipofika kule kwa
Pilato Pilato ni liwali

[Chorus]
Yule Yuda kamwambia
Wayahudi akisema
Nitakaye mbusu ndiye huyo
Mkamateni Mkamateni x2

[5]
Walimpeleka tena kwenda kwa Pilato
Alihukumiwa kupigwa mijiledi
Alipokwisha kupigwa mijiledi
Ndipo kasulubiwa

[Chorus]
Yule Yuda kamwambia
Wayahudi akisema
Nitakaye mbusu ndiye huyo
Mkamateni Mkamateni x2