Katika Mji Wa Tarso

[1]
Katika mji wa Tarso
Mji wake vikia
Palikua kijana mmoja
Jina lake Sauli

[chorus]
Sauli, Sauli, kijana wa Tarso
Alikuwa mtesi, kaomba barua
Kuwatesa wakristo [X2]

[2]
Sauli alitesa watu
Wanaume na wake
Kuwapeleka gerezani
Huko Yerusalemu

[chorus]
Sauli, Sauli, kijana wa Tarso
Alikuwa mtesi, kaomba barua
Kuwatesa wakristo [X2]

[3]
Alipokuwa akienda
Walifika njiani
Akaanguka kifudifudi
Na sauti ikatoka

[chorus 2]
Ni mimi [X2] ni Bwana, unayenitesa leo
Haleluya, simama uende mjini
Ukapate wokovu [X2]