KATIKA BUSTANI

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

KATIKA BUSTANI

[1]
Katika bustani ya Edeni
Kulikuwa na watu wawili;
Mmoja jina lake ni Adamu na mke jina Hawa.

Kaini - Ulikuwa ni mwana wa Adamu
Kaini - Mbona umemuua ndugu yako
Ee, Kaini damu ya ndugu yako
Inanitesa Kaini nitakulaani.

[2]
Siku moja Kaini na Abeli,
Walikwenda kumuomba Mungu;
Sala za Abeli zakubaliwa, Kaini zakataliwa.

[3]
Hata leo wako Kaini wengi,
Katika ulimwengu wa pesa,
Wadanganyifu mbele za Mungu, kwa matendo yao.