Karibu Nawe, Ee Mwokozi

[1]
Karibu nawe, Ee Mwokozi,
Univute Bwana wa thamani;
Unikaribishe moyoni,
Uniweke kwako salamani,
Uniweke kwako salamani.

[2]
Karibu nawe, sina kitu,
Sikuiletea sadaka kuu;
Nakujitolea kabisa,
Kwa damu nipate kutakaswa,
Kwa damu nipate kutakaswa.

[3]
Karibu nawe, Bwana wangu,
Niliuacha uovo wangu;
Kiburi changu na anasa,
Namtaka Yesu aliye Bwana,
Namtaka Yesu aliye Bwana.

[4]
Karibu nawe, hata mwisho,
Nina salama ndani ya Kristo
Mwokozi wangu kwa milele,
Nitakuwa karibu na wewe,
Nitakuwa karibu na wewe.