Baba, Mwana Roho

Language: Swahili
Nyimbo Za Umoja

Baba, Mwana Roho

[1]
Baba, Mwana. Roho, Mungu Mwenye enzi
Kila tukiamka tunakuabudu
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi
Ewe Utatu, tunakusifu

[2]
Baba, Mwana, Roho wakuaminio
Wanakutolea shukurani zao
Wakusujudia malaika nao
Wewe U mwanzo, nawe U mwisho

[3]
Baba, Mwana, Roho sisi tu gizani
Utukufu wako hauoni kosa
U Mtakatifu, nawe U mapenzi
U peke yako, mwenzio huna

[4]
Baba, Mwana, Roho, Mungu Mwenye enzi
Ulivyoviumba vyote vyakusifu
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi
Ewe utatu, tunakusifu