YESU UJE KWETU

[1]
Umetuahidi kwamba wawili watatu , Kwajina lako wakija,
Utabariki; Kwa hivi leo twapiga magoti nyumbani pako.

Chorus
Yesu uje kwetu Utubariki;
Yesu uje kwetu Uwe karibu.

[2]
Umekuwa nasi siku nyingine, Tunakuhitaji mpaka mwisho.
Uje Mwokozi, tupe neema; ‘Tusikie Yesu, utubariki.

[3]
Uje utawale sauti zetu: Nyimbo, nazo sala uziagize;
Imani izidi, ikamilike; Pendo liwe safi, na njia nuru.

01[3]