SAUTI NI YAKE BWANA

[1]
Sauti ni yake Bwana, ‘Kwenda nani tayari?‘
Mavuno yanakawia, Nani atayavuna?
Kwa kudumu anaita, Zawadi atatoa;
Nani atakayejibu, ‘Nipo Bwana nitume.‘

[2]
Kama huwezi safari, Hata nchi za mbali,
Pana watu karibuni, Wasiomjua Yesu;
Kama huwezi kusema, Jinsi ya malaika,
Waweza kuutangaza, Upendo wa Mwokozi.

3
Ingawa huwezi kuwa, Mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu, Nafasi ya uzima;
Kwa sala na kwa sadaka, Watoa msaada,
Kama Harun mwaminifu, Kuinua mikono.

[4]
Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, ‘Hakuna kazi kwangu‘.
Kwa furaha anza kazi, Ile aliyokupa,
Ukajibu mara moja, ‘Nipo Bwana nitume‘.

10[7]