ALILIPA BEI

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

ALILIPA BEI

[1]
Yesu anasema, ‘Wewe huna nguvu,
Kesha ukaombe, Na uje, Mwanagu.‘

Chorus
Alilipa bei, Nawiwa naye;
Dhambi ilitia waa, Aliiondoa.

[2]
Bwana, nimeona, Uwezo wako tu,
Waweza `takasa Mioyo michafu.

[3]
Sina kitu chema, kudai neema,
Hivi nitafua, Mavazi kwa damu.

[4]
Ninaposimama, Juu ya mawingu,
Taji nitaweka, Miguuni pa Yesu.

11[9]