TANGU KUAMINI

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

TANGU KUAMINI

[1]
Ninao wimbo mzuri, Tangu kuamini;
Wa mkombozi, Mfalme, Tangu kuamini.

Chorus
Tangu kuamini, Jina lake `tasifu,
Tangu kuamini, Nitalisifu Jina lake.

[2]
Kristo anitosha kweli, Tangu kuamini,
Mapenzi yake napenda, Tangu kuamini.

[3]
Ninalo shuhuda sawa, Tangu kuamini,
Linalofukuza shaka, Tangu kuamini.

[4]
Ninalo kao tayari, Tangu kuamini,
Nililorithi kwa Yesu, Tangu kuamini.

03[2]