JINA LA YESU SALAMU

[1]
Jina la Yesu, salamu! Lisujidieni,
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni
Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi mpeni

[2]
Enzi na apewe kwenu, watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni
Mkuzeni Bwana wenu, Na enzi mpeni

[3]
Enyi mbegu ya rehema nanyi msifu;
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni
Mmeponywa kwa neema, Na enzi mpeni

[4]
Wenye dhambi kumbukeni ya msalabani
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni
Kwa furaha msifuni, Na enzi mpeni.

[5]
Kila mtu duniani msujudieni
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni
Kote-kote msifuni, Na enzi mpeni.

[6]
Sisi na wao pamoja tu mumo sifani.
Milele sifa ni moja, na `mpeni`
Milele sifa ni moja, na `enzi mpeni`

00[4]