MWUMBAJI , MFALME

[1]
Mwumbaji, Mfalme, Vitu vyote vyako;
Ni kwa ukarimu wako; Ninabarikiwa,
Ni kwa ukarimu wako, Ninabarikiwa.

[2]
Uliyeniumba, Nakutegemea;
Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu,
Sina budi kuzisifu Hisani zako kuu.

[3]
Nitatoa nini? Kwanza vyote vyako,
Upendo wako wadai Moyo wa shukrani,
Upendo wako wadai Moyo wa shukrani.

[4]
Nipewe neema, Niwe na uwezo
Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu,zako,
Wa kuishi kwako, Bwana: Siku zangu,zako.

00[9]