HUNIONGOZA MWOKOZI

[1]
Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo, ataniongoza papo.

Chorus
Kuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye Kristo aniongozaye.

[2]
Pengine ni mashakani nami pengine rahani;
Ni radhi, ijapo yote, yupo nami siku zote.

[3]
Mkono akinishika kamwe sitanung`unika;
Atakachoniletea ni tayari kupokea.

[4]
Nikiisha kazi chini sitakimbia mauti;
Kuishinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba.

15[1]