NATAKA NIMJUE YESU

[1]
Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

Chorus
Zaidi, zaidi,nimfahamu Yesu
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

[2]
Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia
Anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.

[3]
Nataka tena zaidi, daima kupambanua
Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza.

[4]
Nataka nikae naye, kwa mazungumzo matamu.
Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake.

05[4]