YESU FURAHA YA MOYO

[1]
Yesu, furaha ya moyo!Hazina ya pendo, na nuru.
Yote yatupendezayo, yasilinganishwe nawe.

[2]
Kweli yako ya daima, wawajibu wakuitao,
Ni siku zote u mwema kwao wakutafutao.

[3]
U Mkate wa uzima, kupokea ni baraka,
Twanywa kwako u kisima roho zikiburudika.

[4]
Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia;
Twakushika kwa imani, nawe watubariki.

[5]
Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima;
Giza ya dhambi fukuza uwe mwanga wa uzima.

02[3]