WEWE UMECHOKA SANA

[1]
Wewe umechoka sana? Wataka raha?
Kwake Yesu utapata - Msaada.

[2]
Alama anazo Yeye? Sana! Makovu
Ya mikono, na miguu, Na mbavu.

[3]
Naye amevikwa taji Kichwani Mwake?
Taji, kweli, alivikwa - Miiba!

[4]
Huku nikimfuata, Nipate nini?
Maonjo nje, na ndani Amani.

[5]
Kwamba namwandama yeye, Mwisho ni nini?
Kurithi furaha naye - Milele.

11[2]