UJE UKOMBOZI

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

UJE UKOMBOZI

[1]
Unisikie ninapolia, Uje. M-kombozi;
Moyo wangu hukutazamia, Uje. M-kombozi.

Chorus
Nimepotea mbali na kwangu, Nimetanga peke yangu;
Unichukulie sasa kwako: Uje M-kombozi.

[2]
Sina pahali pa kupumzika, Uje M-kombozi
Unipe raha, nuru, uzima, Uje M-kombozi.

[3]
Nimechoka, njia ni ndefu Uje, M-kombozi
Macho yako kuona nataka, Uje M-kombozi.

[4]
Bwana daima hutanidharau, Uje, M-kombozi
Kilio changu utanijibu, Uje, M-kombozi.

00[8]