TWAMSIFU MUNGU

[1]
Twamsifu Mungu, Mwana wa upendo
Aliyetufia na kupaa juu.

Chorus
Aleluya! Usifiwe, Aleluya! Amin;
Aleluya! Usifiwe, utabariki.

[2]
Twamsifu Mungu, Roho mtakatifu,
Akatufunulia Mwokozi wetu.

[3]
Twamsifu Mwana, aliyetufia
Ametukomboa na kutuongoza.

[4]
Twamsifu Mungu wa neema yote
Aliyetwaa dhambi, akazifuta.

[5]
Twamshe tena, tujaze na pendo.
Moyoni uwashe moto wa Roho.

00[2]