TWAE WANGU UZIMA

[1]
Twae wangu uzima, Sadaka ya daima;
Twae saa na usiku, Zikutukuze huku.

[2]
Twae mikono nayo, Ifanye upendavyo,
Twae yangu miguu, Kwa wongozi wako tu.

[3]
Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu;
Itwae na midomo, Ijae neno lako.

[4]
Twae dhahabu pia, Na yote ya dunia;
Twae yangu hekima, Upendavyo tumia.

[5]
Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu;
Twae moyo; ni wako, Uwezo makazi yako.

[6]
Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu;
Twae kabisa nafsi, Niwe wako halisi

14[6]