TUKIMGOJEA

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

TUKIMGOJEA

[1]
Sijui atakapokuja, Mchana au usiku;
Labda sa-a ya alasiri. Pengine ni alfajiri.
Hutwambia tuwe tayari, Ta-a zetu tusizime;
Ili ajapo atukute; Tuwe tukimngoja Yeye.

Chorus
Tu---kimngoje---a, (Kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu---kimngoja---a, (Kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu---kimngoja---a, (Kukesha, tunakungoja Wewe)
Twakesha, twamngoja Yeye.

[2]
Nakumbuka huruma zake, Bei ya wokovu wetu;
Aliacha nyumba tukufu Awafilie wabaya.
Ninadhani itampendeza, Kama sisi watu wake,
Tukionyesha pendo letu, Tuwe tukimngoja Yeye.

[3]
Ee Yesu, Mwokozi mpendwa, Wajua nalihifadhi
Tumaini la kukuona. La kukaribishwa nawe.
Ukija kwa watu wengine, Kama mhukumu wao,
Kwangu utakuwa rafiki, Nakesha, nakungojea.

17[4]