TENA, MWOKOZI, TWALITUKUZA JINA LAKO

[1]
Tena, Mwokozi, twalitukuza jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani, Kabla hatujakwenda nyumbani.

[2]
Tupe amani njiani mwetu, Wewe umwanzo, umwisho wetu;
Dhambini kamwe isiingie Midomo ikutaye wewe.

[3]
Utupe amani usiku huu, Ili gizani kuwe nuru kuu.
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana. Usiku nisawa na mchana.

[4]
Tupe amani ulimwenguni Ndiyo dawa yetu majonzini;
Na ikitwita sauti yako, Tupe amani milele kwako.

02[7]