TAAMINI NITII PIA

[1]
Namwandama Bwana kwa alilonena, Njia zangu huning`azia;
Na nikimridhisha atanidumisha, Taamini nitii pia.

Chorus
Kuamini, Njiani pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu: Amini ukatii.

[2]
Giza sina kwangu wala hata wingu,Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi, sononeko, basi; Huamini nitii pia.

[3]
Masumbuko yote, sikitiko lote; Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki, vivyo hubariki. Taamini nitii pia.

[4]
Mimi sitajua raha sawasawa Ila yote Yesu kumtoa:
Napata fadhili na radhi kamili, Taamini nitii, pia.

[5]
Nitamfurahia na kumtumaini, Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda; nikitumwa hwenda, Huamini, nitii pia

12[8]