SIOSHWI DHAMBI ZANGU

[1]
Sioshwi dhambi zangu? Bila damu yake Yesu,
Hapendezewi Mungu? Bila damu yake Yesu.

Chorus
Hakuna kabisa Dawa ya makosa
Ya kututakasa ila Damu yake Yesu.

[2]
La kunisafi sina, Ila Damu yake Yesu.
Wala udhuru tena, ila Damu yake Yesu.

[3]
Sipati patanishwa, Bila damu yake Yesu,
Hukumu yanitisha, Bila damu yake Yesu.

[4]
Sipati tumaini, Bila damu yake Yesu,
Wema wala amani Bila damu yake Yesu.

[5]
Yashinda ulimwengu, Iyo, damu yake Yesu,
Na kutufikisha juu, Iyo, damu yake Yesu.

09[7]