SI MIMI, KRISTO

[1]
Si mimi, Kristo astahili sifa; Si mimi, Kristo ajulikane;
Si mimi, Kristo katika maneno Si mimi, Kristo kwa kila tendo

[2]
Si mimi, Kristo, kuiponya huzuni; Kristo pekee, kufuta machozi;
Si mimi, Kristo, kubeba mzigo; Si mimi, Kristo, hupunga hofu.

[3]
Kristo pekee, pasipo kujisifu; Kristo pekee, na nisizungumze
Kristo pekee, na hakuna kiburi; Kristo pekee, sifa yangu ife.

[4]
Kristo pekee, mahitaji atoe Si mimi, Kristo, kisima changu;
Kristo pekee, kwa mwili na kwa moyo. Si mimi, Kristo, hata milele.

01[7]