PIGA PANDA YA INJILI

[1]
Piga panda ya Injili, onyesha watu wote;
Ili anayesikia atubu, aokoke.

Chorus
Piga panda ya Injili, upige kwa nguvu;
Mungu amekuagiza mateka wawe huru.

[2]
Upige vilimani, kwa kila tambarare;
Pande zote, miji yote isikie Injili.

[3]
Uipige mipakani, barabarani pia;
Iwatangazie wote, wanakwitwa na Baba.

[4]
Uipige! Watu wengi wataka wawe huru;
Waambie kwamba Yesu asema ‘Njoni kwangu.‘

06[4]