NJONI KWANGU

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

NJONI KWANGU

[1]
Yesu huita kwa upole mwingi, atwita wewe nami; Moyoni mwetu hungoja, hukesha, Hukungojea wewe.

Chorus
‘Njoni kwangu, Mliochoka, njoni: Yesu huita kwa upole mwingi, Akwita, ‘uje kwangu‘

[2]
Atuombeapo usikawie, Hutuombea sisi; Usidharau wema ma huruma, Huruma kwetu sisi.

[3]
Siku za maisha hupota hima, Hupita kwako, kwangu; Usiku waja, kifo kinakuja, Huja kwako na kwangu.

[4]
Fikiri juu ya upendo wake, Upendo kwako, kwangu; Dhambi zetu amekwisha samehe. Masamaha ni yetu.

10[3]