NITEMBEE NAWE

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

NITEMBEE NAWE

[1]
Nitembee nawe mungu Alivyo tembea Henok;
Mkonop wangu uushike: Unene nami kwa pole;
Ingawa njia siioni, Yesu nitembee nawe.

[2]
Siwezi tembea pekee: pana dhoruba mbinguni;
Mitego ya miguu, elfu; Adui wengi hufichwa;
Uitulize bahari, Yesu nitembee nawe.

[3]
Ukinishika mkono Anasa kwangu hasara;
Kwa nguvu nitasafiri; `Tautwika msalaba;
Hata mji wa Sayuni Yesu nitembee nawe.

01[4]