NITAKUANDAMA KOTE

[1]
Nitakuandama kote, nitakapoagizwa
Wewe ukiniongoza nami nitaandama.

Chorus
Nitakuandama kote, naam, ulinifia;
Kwa neema yako Bwana napenda kuandama.

[2]
Njia ijapoparuza kwa miiba na fujo,
Ulitangulia mbele nami nitaandama.

[3]
Nijapokuta taabu na majaribu kote,
Nakumbuka shida yako, nami nitaandama.

[4]
Nijapoona ukiwa na mateso makali,
Wewe uliyatikiza nami nitaandama.

[5]
Ijapo wanipeleka vilindini mwa giza,
Wewe uliyetikiza nami nitaandama.

13[8]