NINAKUHITAJI

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

NINAKUHITAJI

[1]
Bwana ninakuhitaji! Nimpofu, maskini;
Unishike mkononi, Kwako napata nguvu.

Chorus
Kila saa, kila saa Bwana ninakuhitaji;
Kila saa, kila saa, Unilinde kila saa.

[2]
Univike na mavazi Ya usikivu wako;
Nguo zangu ni machafu, Nazitamani zako.

[3]
Wewe ukiniongoza Nitakwenda salama;
Nenda nami siku zote, U nuru na uzima.

[4]
Na ikiwa m-beleni Sehemu yangu ngumu,
Au ikiwa furaha, Unilinde kila saa.

01[6]