NENA MUNGU

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

NENA MUNGU

[1]
Nena rohoni Yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, ‘Huachwi upweke.‘
Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.

Chorus
Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong`oneza kwa pole wa pendo:
‘Daima utashinda, Uhuru ni wako.‘
Nisikie maneno; ‘Huachwi upweke.‘

[2]
Nena kwa wana wako, waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone mwokozi.

[3]
Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yoko tena, Daima kusifu.

01[5]