NA TUMWABUDU MFALME MTUKUFU

[1]
Na tumwabudu huyu Mfalme,
Sifa za nguvu zake zivume;
Ni ngao, ni ngome, Yeye milele,
Ndizo sifa zake kale na kale.

[2]
Tazameni ulimwengu huu,
Ulivyoumwa, ajabu kuu;
Sasa umewekwa pahali pake,
Hata utimize majira yake.

[3]
Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana,
Twakushukuru, U mwema sana;
Hupewa chakula kila kiumbe,
Kila kitu kila mahali pake.

[4]
Wanadamu tu wanyange sana,
Twakutumaini wewe, Bwana;
Kamwe haupunguiwsako wema,
Mkoombozi wetu, Rafiki mwema.

00[5]