MWOKOZI, KAMA MCHUNGA

[1]
Mwokozi, kama mchunga Utuongoze leo;
Ututume malishoni; Fanya tayari boma.
Bwana Yesu, peke yako Umetuvuta kwako.

[2]
Tu wakouwe rafiki, Uwe mlinzi wetu;
Kundi lako ulilinde, Tusivutwe na dhambi;
Bwana Yesu, tusike, Tukiomba, samehe.

[3]
Umetuahidi kwamba Utakubali watu,
Utawahurumia na Utawapa neema;
Bwana Yesu, tunapenda kuwa wako, mapema.

01[8]