MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU

[1]
U Mtakatifu! Mungu mwenyezi!
Alfajiri sifa zako tutaimba;
U Mtakatifu , Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote hata milele.

[2]
U Mtakatifu! Na malaika
Wengi sana wanakuabudu wote;
Elfu na maelfu wanakusujudu
Wa zamani na hata milele.

[3]
U Mtakatifu! Ingawa giza
Lakuficha fahari tusiione,
U Mtakatifu! Wewe peke yako,
Kamili kwa uwezo na pendo.