MSINGI WA KANISA

[1]
Msingi wa Kanisa Ndiye Yesu Bwana;
Kiumbe chake kipya Akipenda sana;
Kutaka ‘kitafuta Alishuka chini,
Naye kwa haja yake, Akafa Mtini.

[2]
Lina kila kabila Kisha ndiyo moja
Wokovu wake una Mwokozi ndiyo moja;
Uzazi ni umoja. Moja tumaini.
Chakula ni kimoja. Moja tumaini.

[3]
Watu hustaajabu Kwa mashaka yote.
Yaipatayo nje Hata ndani mwote;
Ila watakatifu Humwomba, wakikesha
Usiku ni kilio. Asubuhi raha.

[4]
Mashaka na taabu Hata vita vyake.
Vyangoja matimizo Ya amani yake.
Ndipo kwa macho yetu Twone utukufu
Kanisa ya kushinda itastarehe juu.

19[5]