MLANGO WAZI

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

MLANGO WAZI

[1]
Mlango uko wa wema, Mlango wazi huo:
Yesu ameufungua Na hakuna kufunga

Chorus
Mlango wazi, ajabu, Uliachwa wazi kwangu?
Kwangu, Kwangu? Wazi, wazi kwangu?

[2]
Mlango hukaa wazi Watu waokolewe:
Maskini na matajiri Wa mataifa yote.

[3]
Maadam mlango wazi, Rafiki kaza mwendo;
Msalaba ukubali - Amana ya upendo.

[4]
Msalaba tutabeba Daima, na furaha!
`Pendo wa Yesu hushinda. Tunainama kwake!

1[10]