KWA MAHITAJI YA KESHO

[1]
Kwa mahitaji ya kesho, Sina ombi;
Unilinde nisitende Dhambi leo;
Nisiseme neno baya, Mkombozi,
Nisifikiri uovu, Leo hivi.

[2]
Ningefanya kazi sawa Nakuomba;
Ningekuwa mtu mwema Kila saa;
Mapenzi yako nifanye, Na kutii;
Nitoe mwili dhabihu, Leo hivi.

[3]
Kama leo ningekufa Kwa ghafula,
Nitegemee ahadi Zako Bwana.
Kwa mahitaji ya kesho Sina ombi;
Uniongeze, nishike Leo hivi.

13[1]