KARIBU SANA

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

KARIBU SANA

[1]
Karibu sana univute, karibu sana daima niwe.
Bwana napenda unishike, Unilinde nisitengwe nawe,
Unilinde nisitengwe nawe.

[2]
Karibu sana, sina kitu, Sina sadaka kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa moyo wangu: Uutakase katika damu,
Uutakase katika damu.

[3]
Karibu sana wewe, wewe nami, Nitafurahi kuacha
Dhambi- - Anasa zote na kiburi: Nipe Yesu niliye msulibi,
Nipe Yesu niliye msulibi.

[4]
Karibu sana, hata mwisho. Hata mbinguni nisimamapo:
Daima dawamu niwepo Nitakapoona uso wako,
Nitakapoona uso wako.

03[3]