JINA LA THAMANI

[1]
Jina lake Yesu tamu, Lihifadhi moyoni;
Litakufariji ndugu,Enda nalo popote.

Chorus
Jina la Thamani,
(Thamani) (thamani)
Tumai la dunia
Jina la thamani - - tamu!)
Furaha ya mbinguni.

[2]
Jina la Yesu lafaa Kama ngao vitani.
Majaribu yakisonga, Omba kwa jina hili.

[3]
Jina hili la thamani Linatufurahisha,
Napotukaribisha, Na tunapomwimbia.

[4]
Mwisho wa safari yetu Tutakapomsujudu.
Jina hili tutasifu Furaha ya mbinguni.

02[8]