HADITHI KISA YESU

[1]
Nipe habari za Yesu, Kwangu ni tamu sana;
Kisa chake cha dhamani Hunipendeza sasa.
Jinsi malaika wengi walivyoimba sifa,
Alipoleta amani kwa watu wa dunia.

Chorus
Nipe habari za Yesu, Kaza moyoni mwangu;
Kisa chake cha dhamani Hunipendeza sasa.

[2]
Kisa cha alivyofunga Peke yake jangwani.
Jinsi alivyolishinda jaribu la shetani;
Kazi aliyoifanya, Na siku za huzuni,
Jinsi walivyomtesa: Yote ni yaajabu!

[3]
Habari za msalaba Aliposulubishwa:
Jinsi walivyomzika Akashinda kaburi.
Kisa chake cha rehema. Upendo wake kwangu,
Aliye toa maisha Nipokee wokovu.

03[4]