HACHA, MANENO MABAYA YASITOKE

[1]
Hacha, maneno mabaya Yasitoke Kinywani
Moyo mwema uzuie Ndimi, zisichafuke

Chorus
‘Nanyi pendeni‘, Asema Yesu, (mpendane) (mpendane)
Kama mwanzo alivyotupenda:
‘Nanyi pendeni‘, Asema Yesu, (mpendane) (mpendane)
Wana, tiini amri hii. (amri heri hii).

[2]
Pendo ni mtakatifu; Urafiki: mzuri:
Visiharibike mara Kwa kunena vibaya.

[3]
Tusinene kwa hasira, Inazaa huzuni.
Pendo lako, ee Mwokozi, Inatosha tushinde.

150