ANISIKIAYE

Language: Swahili
Nyimbo Za Kikristo

ANISIKIAYE

[1]
Anisikiaye, aliye yote, sana litangae, wajue wote,
Duniani kote neno wapate, atakaye na aje!

Chorus
Ni ‘atakaye,‘ ni ‘atakaye‘; Pwani hata bara, na litangae:
Ni Baba mpenzi alinganaye atakaye na aje.

[2]
Anijiliaye, Yesu asema, asikawe, aje hima mapema;
Ndimi Njia, kweli, ndimi uzima: atakaye na aje!

[3]
Atakaye aje, ndiyo ahadi; atakaye hiyo haitarudi!
Atakaye lake, ni la ahadi! Atakaye na aje.

10[9]