Pote Mashamba Yajaa

[1]
Po pote mashamba yajaa, tele nafaka pevu,
Po pote yang‘aa meupe bondeni na nyandani.

Mwenye mavuno, twasihi upeleke wavuni,
Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.

[2]
Wapeleke uchaoni, waende na jotoni,
Hata jua lishukapo wakusanye ko kote.

[3]
Enyi wakazi wa Bwana yaleteni mazao,
Na jioni ingieni kwake na furaha kuu.