mahali pa maji

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

mahali pa maji

[1]
Mahali pa maji mazuri maji ya uzima;
Anapotungojea Yesu tutakaribishwa.

Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima;
Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima.

[2]
Tunapochoka safarini, tamu kupumzika
Panapo maji ya uzima yatufurahisha.

[3]
Una kiu? uje kwa Yesu, utaburudishwa;
Yesu yu maji ya uzima, unywe, uokoke.