Askari

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Askari

[1]
Twendeni askari, watu wa Mungu; Yesu yuki mbele tumwandame juu
Ame tangulia Bwana vitani, Twende mbele kwani ndiye amini.

Twendeni askari watu wa Mungu
Yesu yuko mbele, tumwandame juu.

[2]
Jeshi la shetani, likisikia Jina la Mwokozi, litakimbia;
Kelele za shangwe zivume pote; Ndugu, inueni zenu sauti.

[3]
Kweli kundi dogo, watu wa Mungu, La mababa yetu ni letu
Fungu. Hatutengwi nao, moja imani tumaini moja, na moja dini.

[4]
Haya mbele watu nasi njiani, Inieni myoyo, nanyi sifuni;
Heshima na sifa yake mfalme, Juu hata chini sana zivume.