Mahali Pazuri Mno

[1]
Pana mahali pazuri mno,
Twapaona kwa mbali sasa;
Baba yetu angoja pale,
Amepanga makao yetu.

Kitambo tu bado,
Tutakutana ng‘ambo pale.
Kitambo tu bado,
Tutakutana ng‘ambo pale.

[2]
Tutaimba pale kwa moyo
Nyimbo tamu za wenye heri.
Na rohoni hatutaona
Tena haja ya kupumzika.

[3]
Kwa Baba yetu mkarimu
Tutatoa shukrani sana,
Kwa kipaji cha pendo lake
Na baraka anazotupa.