Unipendaye

Language: Swahili
Nyimbo za Kristo

Unipendaye

[1]
Yesu unipendaye kwako nakimbilia,
Ni wewe unitoshaye mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni mwako maisha yangu;
Nifiche bandarini, wokoe moyo wangu.

[2]
Ngome nyingine sina; nategemea kwako;
Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuaminia, mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia, vitani wani tosha.

[3]
Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako,
Niwapo muhitaji, utanijaza vyako;
Nao waangukao wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao, uongoze vipofu.

[4]
Bwana umeniosha moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha ya patikana kwako;
Kwako Bwana naona kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana, bubujika daima.